Wakili Peter Kibatala atoa taarifa kuhusu Niffer kuwa salama na taratibu za kumsaidia kisheria zinaendelea

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: wakili-peter-kibatala-atoa-taarifa-kuhusu-niffer-kuwa-salama-taratibu-kumsaidia-kisheria-951-rickmedia

Jopo la mawakili wa mfanyabiashara #Niffer, likiongozwa na Wakili Peter Kibatala, limethibitisha kuwa #Niffer yuko salama.

Wamesema matukio yaliyotokea hivi karibuni yameathiri uwezo wao wa kuendelea na majukumu ya kisheria, lakini wamewahakikishia wananchi kuwa mrejesho wa kisheria utatolewa hivi karibuni.

Kwa upande mwingine, Kamanda Muliro ameeleza kuwa Niffer anatuhumiwa kuhamasisha vurugu, kuharibu miundombinu, na kuchoma vituo vya mafuta wakati wa siku ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.