Mahakama mjini Aachen, Ujerumani, imemhukumu Muuguzi mmoja wa Kiume mwenye umri wa miaka 44 (Jina Halijawekwa Wazi) kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya wagonjwa 10 na kujaribu kuwaua wengine 27 kwa kutumia sindano za sumu.
Mauaji hayo yalifanyika kati ya Desemba 2023 na Mei 2024 katika hospitali ya Wuerselen, karibu na Aachen.
Waendesha mashtaka walimtuhumu kwa kuchezea maisha ya wagonjwa, huku upande wa utetezi ukitaka aachiliwe huru.
Mahakama ilimpata na hatia na kuamuru atumikie kifungo cha maisha gerezani.