Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeahirisha hadi Novemba 10, 2025 kusikiliza shauri lililofunguliwa dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na wengine, linalolenga kumtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, afikishwe mahakamani.
Uahirisho huo umetokana na ombi la upande wa Jamhuri la kupewa muda zaidi kuandaa na kuwasilisha kiapo cha kujibu hoja za walalamikaji.