Mata yaanza kuwaondoa watoto mitandaoni

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

10 hours ago
rickmedia: mata-yaanza-kuwaondoa-watoto-mitandaoni-649-rickmedia

Kampuni ya Meta imesema imeanza kuondoa akaunti za vijana walio chini ya umri wa miaka 16 kutoka kwa mitandao yao ya kijamii nchini Australia kuelekea marufuku iliyotangazwa na Serikali ya nchi hiyo kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 hawataruhusiwa kuwa na akaunti katika mitandao ya kijamii kama Tiktok, Facebook, Youtube na Instagram.

Sheria hiyo inaanza kutekelezwa rasmi Jumatano ijayo.

Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ilitangaza mwezi uliopita kuwa imeanza kuwafahamisha watumiaji wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 15 kwamba akaunti zao zitaanza kufungwa kuanzia Desemba 4, 2025.

Takriban watumiaji 150,000 wa Facebook na akaunti 350,000 za Instagram wanatarajiwa kuathirika.

Mitandao ya Threads, sawa na X, zinaweza kupatikana tu kupitia akaunti ya Instagram.