Mfanyabiashara Niffer na Mika waachiwa huru

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

16 hours ago
rickmedia: mfanyabiashara-niffer-mika-waachiwa-huru-304-rickmedia

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewafutia mashtaka na kuwaachia huru mfanyabiashara wa vipodozi Jenifer Jovin (26) (Niffer) na Mika Lucas Chavala, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhaini.

Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 3, 2025 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, baada wakili wa Serikali, Titus Aron kuileleza Mahakama hiyo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.