Loading...

Mwendokasi za Mbezi kwenda Kivukoni, Gerezani kuishia Magomeni Mapipa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 weeks ago
rickmedia: mwendokasi-mbezi-kwenda-kivukoni-gerezani-kuishia-magomeni-mapipa-647-rickmedia

Watumiaji wa mabasi ya mwendokasi yanayofanya safari zake kutoka Mbezi kwenda Kivukoni na Gerezani wamejikuta wakiishia Magomeni Mapipa kutokana na eneo la Jangwani kufungwa kutokana na mafuriko ya mvua zilizonyesha usiku wa leo.

Taarifa iliyotolewa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) leo Juni 19, 2024 imesema kutokana na eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam kujaa maji imewalazimu kuishia Magomeni Mapipa.

“Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka - DART unawaarifu watumiaji wa mabasi ya Mfumo wa DART kuwa leo, Juni 19, 2024, Barabara ya Jangwani imefungwa kutokana na mafuriko. Mabasi kwa njia za Kimara hadi Kivukoni na Gerezani yanaishia Magomeni Mapipa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Eneo la Jangwani limeendelea kuwa changamoto kila mvua zinaponyesha na kusababisha Barabara ya Morogoro kufungwa kutokana na mafuriko. Hata hivyo, tayari Serikali imeshaweka mipango ili kulitafutia suluhu ya kudumu kwa kujenga daraja.