Serikali imetangaza hali ya dharura na amri ya kukaa ndani (kuanzia Saa 12 Jioni - 11 Asubuhi) hadi Machi 6, 2024 kwa Wakazi wa eneo la Ouest linalojumuisha Mji Mkuu katika jitihada za kukabiliana na vurugu kwenye Magereza Mawili zilizowawezesha Maelfu ya Wafungwa kutoroka Machi 3, 2024.
Vurugu hizo zilizosababisha Vifo vya takriban Watu 12 huku Wafungwa zaidi ya 4,000 wakitoroka, zimesababishwa na magenge ya Uhalifu yanayoongozwa na Askari wa Zamani (Jimmy Cherizier) wanaomshinikiza Waziri Mkuu, Ariel Henry kutoka Madarakani.
Ikumbukwe, Wiki iliyopita Ariel Henry alikuwa Kenya kusaini makubaliano ya kutuma Polisi kuongoza jukumu la kurejesha Sheria na Utaratibu kwa msaada wa Umoja wa Mataifa (UN) katika taifa hilo lililoathiriwa na Magenge ya Uhalifu.