Profesa Abraham Kithure Kindiki ameapishwa na Msajili wa Mahakama, Winfrida Mokaya kuwa Naibu Rais mbele ya Jaji Mkuu katika hafla inayoandaliwa katika eneo la KICC, Nairobi.
Amechukua nafasi iliyoachwa na Rigathi Gachagua ambaye aliondolewa Madarakani na Bunge baada ya kukutwa na hatia ya makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya Madaraka na kukiuka Katiba.