Bunge limeidhinisha Muswada unaosimamia Usalama wa maumbile, ukilenga kushughulikia hatari inayoweza kutokea kwenye Matumizi ya GMOs ili kulinda Bioanuwai na kuhifadhi Mazingira.
Kuidhinishwa kwa Muswada huo kunafuatia Rwanda kujiunga na Kituo cha Kimataifa cha Uhandisi wa Jenetiki na Bioteknolojia (ICGEB) Julai 19, 2022
Hivi karibuni Mahakama ya Mazingira Nchini Kenya nayo ilihalalisha Matumizi ya Mbegu za GMO kwa Matumizi ya Binadamu baada ya Wanaharakati kushindwa kudhibitisha uwepo wa Madhara ya Kiafya.
GMO ni Mbegu za Mazao zinazobadilishwa Vinasaba (Genetics) ambazo huweza kukabiliana na Wadudu, na kukua katika Hali mbaya za Hewa.