Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu walirusha kwa parachuti tani 25 za msaada wa Chakula ndani ya Ukanda wa Gaza

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: jordan-umoja-falme-kiarabu-walirusha-kwa-parachuti-tani-msaada-chakula-ndani-ukanda-886-rickmedia

Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu walirusha kwa parachuti tani 25 za msaada wa Chakula ndani ya Ukanda wa Gaza siku ya Jumapili, katika zoezi lao la kwanza la anga kwa miezi kadhaa.

afisa wa Jordan amesema Nchi hiyo imethibitisha kuwa imefanya mara tatu zoezi la kurusha misaada kwa kutumia ndege juu ya Gaza, ikiwemo moja kwa ushirikiano na

Umoja wa Falme za Kiarabu.

Picha zinazotoka Gaza katika siku za hivi karibuni zikionyesha watoto waliokonda sana zimeibua ukosoaji

mkubwa wa kimataifa dhidi ya Israel, ikiwemo kutoka kwa washirika wake wa karibu, ambao wamekuwa wakitoa wito wa kusitishwa kwa vita na janga la kibinadamu lililotokana na mzozo huo.