Mastaa Marufuku Kutangaza Pombe, Kenya

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 months ago
rickmedia: mastaa-marufuku-kutangaza-pombe-kenya-134-rickmedia

Watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii, mastaa, na wanahabari Nchini Kenya wamepigwa marufuku kuidhinisha, kutangaza, au kupigia debe matumizi ya pombe, dawa za kulevya, na vitu vinavyohusiana navyo.

Sera mpya ya #NACADA pia inawahusu wachekeshaji, wanamichezo, na watu mashuhuri katika tasnia ya burudani na michezo, kama sehemu ya juhudi za kupunguza mvuto wa matumizi ya vileo miongoni mwa vijana.