Mwijaku Aliwa Kichwa Ubunge wa Mvomero

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: mwijaku-aliwa-kichwa-ubunge-mvomero-521-rickmedia

Mtangazaji maarufu na Mwana burudani, Mwijaku, amekosa nafasi ya kupenya kwenye orodha ya wagombea wanane waliopitishwa rasmi kuwania ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge wa Jimbo la Mvomero, mkoani Morogoro, katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, CCM imekamilisha hatua ya awali ya mchujo wa majina ya wanachama waliojitokeza kuomba kugombea nafasi hiyo, ambapo majina yaliyopenya yamechaguliwa kwa kuzingatia vigezo vya chama, maadili, uadilifu na uwezo wa kisiasa.