Marekani na Saudi Arabia zimesaini mkataba wa kihistoria wa ushirikiano wa nishati ya nyuklia. Hatua hii inaweza kuipatia Saudi Arabia uwezo wa kurutubisha madini ya yuraniamu katika ardhi yake kwa ajili ya kuzalisha nishati, badala ya kutegemea kuagiza mafuta kutoka nje.

Mkataba huu umeafikiwa katikati ya mvutano mkubwa wa kisiasa na usalama Mashariki ya Kati, ikiwa ni siku mbili tu baada ya kundi la Houthis nchini Yemen ambalo ni mshirika wa Iran kutangaza kuweka vikwazo vya usafiri wa baharini dhidi ya Ufalme huo