Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates - UAE) ambapo ni kitovu cha Biashara na Viwanda katika Ukanda wa Mashariki ya Kati, umetangaza kusitisha uhusiano wa Kidiplomasia dhidi ya Israel kufuatia mauaji ya Wafanyakazi saba wa Misaada ya Kibinadamu yaliyotokea Gaza
Inadaiwa Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE imeonesha hasira juu ya tukio hilo na kufikisha ujumbe huo kwa Balozi wa Israel-UAE, Amir Hayek
Wafanyakazi waliouawa katika shambulizi la anga la Israel walikuwa raia wa Uingereza, Poland, Australia, Palestina na wawili wa Marekani na Canada
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema Jeshi lake limewashambulia Watu wasiokuwa na hatia, hilo halikuwa kusudio lao na kuongeza “Inatokea kwenye vita, tunawasiliana na Serikali na tutafanya kila kitu ili jambo hili lisitokee tena.”