Rais Wa Marekani #DonaldTrump ametangaza pendekezo jipya la sera ambalo litaona kila mtoto wa Marekani aliozaliwa kati ya Januari 1, 2025, na Desemba 31, 2028, akipewa akaunti ya uwekezaji ya dola 1,000 (Tsh.Milioni 2.6) kutoka kwa serikali ya shirikisho.
Akaunti hizi za uwekezaji zitakuwa hazitozwi kodi hadi pale fedha zitakapochukuliwa (tax-deferred) na zitahusishwa na utendaji wa jumla wa soko la hisa, ambapo walezi watakuwa na udhibiti wa akaunti hizo hadi mtoto atakapofikia umri wa utu uzima.
Kulingana na #Trump, mpango huu unalenga kuhamasisha uwekezaji na kujenga utajiri wa muda mrefu kwa ajili ya vizazi vijavyo.