Kila mtu amekuwa na mtazamo wake juu ya Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zambia Clatous Chota Chama kujiunga klabu ya Yanga akitokea Simba huku wengi wakidai kuwa CHAMA ameikimbia Simba kwasababu Simba haishiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
Kwa mara ya kwanza Chama amefunguka kuwa hiyo haikuwa sababu kuu ila muda ulifika tu wa yeye kuitumikia klabu ya Yanga. Chama amefunguka kupitia Yanga APP
"Inaweza kuwa sababu moja lakini sio asilimia 100 kuwa nimejiunga yanga ili niweze kucheza klabu bingwa Afrika, nimejiunga Yanga kwasababu niliona ni muda wa kujiunga na Yanga na nataka nifanye Challenge mpya kwenye maisha yangu ya mpira na nafurahia nimejiunga Yanga na jinsi mambo yanavyoenda"