Dullah Mbabe apigwa tena na Eric Katompa wa DR Congo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: dullah-mbabe-apigwa-tena-eric-katompa-congo-229-rickmedia

Bondia Abdallah Pazi “Dullah Mbabe” ameendeleza unyonge kwa kupoteza kwa mara nyingine dhidi ya "Eric Katompa" Raia wa DR Congo katika pambano lisilo la ubingwa la Uzito wa Super Middleweight lililofanyika Mkoani Arusha.

Katompa ameshinda kwa pointi baada ya majaji watatu kumpa ushindi wa Pointi 93-97, 93-97na 92-98.

Akizungumza baada ya pambano, Dullah amesema “Sijui Majaji au Chama cha Ngumi wana nia gani na mimi kwa kuwa nimecheza vizuri na mashabiki wameona kilichotokea.”

Hiyo ni mara ya pili Dullah anapoteza pambano dhidi ya Katompa, awali alipoteza walipokutana Oktoba Mosi, 2021 kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba Jijini Dar es Salaam.