Loading...

Polisi wa Ujerumani wapendekeza bangi badala ya Bia kwa mashabiki

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: polisi-ujerumani-wapendekeza-bangi-badala-bia-kwa-mashabiki-123-rickmedia

Polisi wa Ujerumani wamewataka mashabiki wa soka wa England kutumia bangi badala ya pombe wakati wa michuano ya Euro 2024, iliyoanza jana, Ijumaa Juni 14.

Mamlaka zinaamini kuwa kuvuta bangi kutawafanya mashabiki kuwa watulivu, hivyo kupunguza uwezekano wa tabia za fujo zinazohusishwa na unywaji pombe kupita kiasi.

Ushauri huu wa kipekee umetolewa baada ya kupigwa marufuku kwa bia kali kuelekea mechi yao ya kwanza, England dhidi ya Serbia, siku ya Jumapili ambayo imeonekana kuwa mchezo ulio kwenye hatari kubwa kutokana na historia ya fujo miongoni mwa makundi ya mashabiki wa timu zote mbili.