Simba imeendelea kuwa na mwendo wa kinyonga kwenye Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupata sare ya 0-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy FC Nchini Botswana.
Simba imefikisha pointi 2 wakati Jwaneng ikifikisha pointi 4, timu hizo zimecheza mechi mbili kila moja katika Kundi B.
Mchezo ujao wa Simba utakuwa ugenini tena kukipiga na Wydad AC, Desemba 9, 2023.