A-Z Kajala Afunguka kuhusu Harmonize "Alimsaidia Baba Yangu"/Kuhusu Range Rover.

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 year ago
rickmedia: a-z-kajala-afunguka-kuhusu-harmonize-alimsaidia-baba-yangukuhusu-range-rover-528-rickmedia

Mwigizaji wa filamu Tanzania Kajala Frida ambaye pia alikuwa mpenzi wa Msanii wa muziki Tanzania Harmonize, Leo amefanya mahojiano na wandishi wa habari ambapo amejibu maswali yote ambayo mashabiki zake walitamani kupata majibu.

Moja Kati ya maswali aliyojibu ni juu ya taarifa alizozitoa Harmonize kuwa alikuwa anampa asilimia 10% ya kipato chake, ampapo Kajala Frida amesema ni kweli alikuwa anapewa asilimia hizo japo kuwa alipewa miezi miwili kabla ya wao wawili kuachana na swara la Kajala kujua password ya akaunti za Harmonize za benki amesema kuwa Password za akaunti za benki zinajulikana na vijana wote wa Konde Gang.

Pia Kajala amekili kuwa Harmonize alimsaidia Baba yake mzazi,kuhusu kuuza gari Aina ya Range rover aliyoachiwa na Harmonize baada ya kuachana na kutumia Toyota amejibu Range rover hiyo bado ipo ila anapendelea kutumia gari ya mwanaye(Paula Kajala) Kwa sababu hapendelei kujulikana kama Kajala kila maeneo.

Kajala amekanusha kumnyanyasa Anjella ambaye alikuwa msanii wa Konde Gang na kusema kuwa yeye alikuwa akimpigania Wakati anatoka kwenye record label ya Konde Gang apewe japo gari kutokana na Hali ya afya ya miguu wa msanii huyo.



(Imeandaliwa na Nzaniye Kanubo)