Kwenye mahojiano yake mapya na Kelly Rowland, mwanamuziki Cardi B amefunguka kuhusu changamoto alizokumbana nazo alipojaribu kusaidia wasanii wengine wa kike. Cardi B amesema amekuwa akiwapa ushauri na msaada, lakini baadhi yao walitumia fursa hiyo vibaya.
"Niliwasaidia, niliwapa ushauri, niliwaelekeza jinsi ya kufanya muziki. Lakini mwishowe, baadhi yao walilala na mpenzi wangu," alisema Cardi B
Kauli hii imeibua hisia mbalimbali mtandaoni, huku wengi wakimpongeza kwa ujasiri wake wa kuzungumzia suala hili hadharani. Kwa mujibu wa Cardi B, uaminifu ni jambo muhimu sana kwenye urafiki, hasa kwenye maeneo ya kitaaluma.