Video ya Dababy yazua gumzo sababu ya Mkimbizi wa Ukrain

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: video-dababy-yazua-gumzo-sababu-mkimbizi-ukrain-751-rickmedia

Rapa DaBaby, amezua mzozo mkubwa baada ya video yake mpya ya muziki inayohusiana na kifo cha mkimbizi wa Ukraine, Iryna Zarutska. Video hiyo inarudia tukio la kikatili lililotokea wakati Zarutska alipokuwa akirudi nyumbani huko North Carolina, ambapo aliuliwa kwa kisu na mtu asiyejulikana.

Tofauti na kisa halisi, video ya DaBaby inaonyesha mwisho mbaya, ikianza na kipande cha habari cha kweli kilichoripoti kifo cha Zarutska, pamoja na picha za usalama kutoka tukio hilo la Agosti 22.

Video hiyo imeibua maoni mchanganyiko kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wengine wakiwa na maoni chanya na wengine wakilaumu hatua hiyo ya DaBaby.