Miss Rwanda Akamatwa Akiendesha Gari Akiwa Amelewa

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

3 days ago
rickmedia: miss-rwanda-akamatwa-akiendesha-gari-akiwa-amelewa-935-rickmedia

Polisi nchini Rwanda imetangaza kumkamata Mlimbwende Divine Muheto kwa tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa kitu ambacho adhabu yake ni faini ya Laki Moja na nusu pesa ya Rwanda na kufungwa Gerezani kwa siku tano.

Katika tangazo hilo linasema kuwa Miss Divine Muheto alikuwa anaendesha gari kinyume na sheria kutokana na kutokuwa na leseni ya udereva.

Muheto hadi kufikia sasa hajazungumzo kitu chochote kuhusiana na shutuma hizo.

Muheto mwenye umri wa miaka 21 alifahamika mwaka wa 2022 baada ya kubeba taji la Miss Rwanda kabla ya Serikali ya Rwanda kuyapiga marufuku mashindano hayo kwa madai ya kuwepo kwa shutuma za unyanyasaji kutoka kwa waandaaji.

Kukamatwa kwa Divine Muheto kumekuja baada ya hivi karibuni mlimbwende huyo kuripotiwa kupata ajali akiwa amelewa.