Mtoto wa staa wa muziki Nchini Tanzania, Omary Ally Mwanga,maarufu kama Marioo na Mwanamitandao Paula Kajala Masanja, Amara amefikisha Nusu mwaka tangu kuzaliwa kwake.
Mapema Januari 19,2024 video za Paula akiwa Hospitali na ujauzito zilithibitiha mrembo huyo kuwa ni mjamzito licha ya kuwa mara kadhaa alikuwa akikana kuwa na ujauzito. Hata hivyo Mwezi Aprili mwaka huu wawili hao walifanya ‘Baby Shower’ kwaajili ya kutambulisha jinsia ya mtoto wao.
Aprili 2023 Marioo na Paula walitajwa kuwa kwenye mahusiano hii ni baada ya Paula kuachana na msanii wa muziki Rayvanny.