Maelfu ya Waisraeli waliandamana nchini kote jana Jumapili, Agosti 17, wakidai kumalizika kwa vita vya Gaza na kuachiliwa kwa mateka 50 waliobaki, ambapo takriban 20 wanahofiwa bado wako hai. Waandamanaji walifunga barabara na kukusanyika nje ya makazi ya wanasiasa na makao ya jeshi, hali iliyosababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliwaambia mawaziri wake kuwa vita vitaendelea hadi Hamas ipokonywe silaha na Gaza ibaki haina uwezo wa kijeshi. Alikosoa wito wa kumaliza vita bila ushindi dhidi ya Hamas, akisema unahatarisha usalama wa Israel na kuchelewesha kuachiliwa kwa mateka.
Mandamano hayo yameibuka baada ya video za mateka waliodhoofika kusambazwa na makundi ya wanamgambo na Israel kutangaza mashambulizi mapya