Polisi Wamuachia Mfungwa mwenye Kifungo cha Miaka 5 Kimakosa

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

8 hours ago
rickmedia: polisi-wamuachia-mfungwa-mwenye-kifungo-cha-miaka-kimakosa-416-rickmedia

Mamlaka za Texas zinamsaka Troy Dugas (36) baada ya kuachiliwa kimakosa kutoka gerezani tarehe 17 Agosti saa 10:30 alfajiri. 

Dugas alikuwa anatakiwa kuanza kutumikia kifungo cha miaka 5 kwa kosa la kumpiga mwanafamilia na kifungo cha miaka 2 kwa kosa la kukimbia polisi.

Jeshi la Polisi la Kaunti ya Harris limesema makosa ya kiutendaji ya maafisa wa jela yalisababisha kuachiliwa kwake baada ya kesi nyingine dhidi yake kufutwa. Dugas anaelezewa kuwa mwanaume mweusi, urefu futi 6’1 na uzito pauni 215.

Mamlaka zimeomba yeyote atakayemuona kumpigia 911 mara moja.