Loading...

Shakira amaliza kesi nje ya Mahakama kwa kulipa faini Tsh. Bilioni 20

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

7 months ago
rickmedia: shakira-amaliza-kesi-nje-mahakama-kwa-kulipa-faini-tsh-bilioni-67-rickmedia

Nyota wa Muziki wa Pop na Raia wa Colombia, Shakira amefikia makubaliano na Waendesha Mashtaka wa Hispania kumaliza shauri la kukwepa Kodi kwa kulipa Euro Milioni 7.5 (Tsh. Bilioni 20.4) kabla kesi ya msingi haijaanza kisikilizwa Mahakamani.

Awali, Shakira alikataa kulipa Faini hiyo alipoambiwa achague kulipa kiwango hicho ili mambo yaishe au shauri liende Mahakamani na akishindwa kesi kuna kifungo cha Miaka 8 jela na Faini ya Euro 23.8m (Tsh. Bilioni 65), akachagua Mahakamani kabla ya kubadili mawazo baadaye.

Shauri la Msingi lilikuwa kukwepa Kodi ya Euro Milioni 14.5 (Tsh. Bilioni 39.4) lililowasilishwa Mahakama ya Barcelona. Shakira ameamua kulipa kwa maslahi ya Watoto wake.