Serikali ya China imepanga kuanza ujenzi wa bwawa kubwa zaidi la kuzalisha umeme duniani, litakalojengwa kwenye ukingo wa mashariki wa eneo la Tibet. Mradi huo mkubwa unakadiriwa kugharimu takribani Dola za Marekani bilioni 170, sawa na Shilingi trilioni 443.5 za Tanzania.
Bwawa hilo, ambalo litajumuisha vituo vitano vya kufua umeme, linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya kilowati bilioni 300 za umeme kila mwaka, na kukamilika ifikapo mwaka 2033.
Mradi huu ni sehemu ya juhudi za China kuongeza uzalishaji wa nishati safi na kupunguza utegemezi wa makaa ya mawe, huku ukichochea maendeleo ya miundombinu na kiuchumi katika maeneo ya pembezoni.