Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kitendo cha Serikali kupitisha Kodi hiyo kitawarudisha nyuma Wafanyabiashara wanaotarajia kufungua Maduka siku za mbele.
Kauli ya Mbowe inakuja baada ya Kampuni ya META inayomiliki Mitandao ya Facebook, Instagram, WhatsApp na Thread kutangaza kuwa Wafanyabiashara wanaotangaza bidhaa zao kupitia Mitandao wataanza kukatwa 18% ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuanzia Desemba 1, 2023.
Mbowe amesema "Serikali inayotoa msamaha wa kodi kwa Kampuni zenye mitaji ya Mabilioni, imegoma kuwapatia Wananchi wake ahueni. Serikali inaendelea kujaza kodi kila sehemu huku ikishindwa kudhibiti wizi wa kodi ambazo Watanzania wamelipa na CAG amethibitisha hilo kwa Miaka mingi".