Jeshi la Polisi Mkoani Njombe linamshikilia Mtoto wa Miaka 12 akituhumiwa kumlawiti Mtoto mwenzake (10), Mwanafunzi wa Darasa la Nne kwa muda mrefu kiasi cha kumuathiri Kiafya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga amesema tukio hilo limetokea Mjini Makambako ambapo Mtuhumiwa aliacha Shule akiwa Darasa la Sita na amekuwa akimfanyia mwenzake Ukatili huo kwa muda mrefu akimlaghai kwa kumpatia Fedha.