Mchengerwa, amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wa Halmashauri ili kupisha Uchunguzi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 weeks ago
rickmedia: mchengerwa-amewasimamisha-kazi-wakurugenzi-wawili-halmashauri-ili-kupisha-uchunguzi-116-rickmedia

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa. Mhe; Mohamed Mchengerwa, amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wa Halmashauri ili kupisha Uchunguzi uendelee.

Wakurugenzi hao ni Bi.Butano Nuru Ndalahwa wa Halmashauri ya wilaya ya kibaha mkoani pwani na mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Ifakara mkoani Morogoro Bi.lena martin nkaya 

Pia Mhe; waziri amechukua hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi hao mara baada ya kupokea taarifa ya awali kutoka Kwa timu iliyoiunda kwaajil ya kupeleleza tuhuma za wakurugenzi hao kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo katika Halmashauri zao Kwa nyakati tofauti.

Timu hiyo iliundwa na katibu mkuu Kwa maelekezo ya waziri Mchengerwa, na imebaini mapungufu kutoka Kwa wakurugenzi hao.

Aidha mhe; waziri amewasisitiza wakurugenzi wote wa mamlaka za serikali za mitaa kutekeleza majukumu Yao kikamirifu, ikiwa ni kusimamia miradi ya kimaendeleo nchini.


(Imeandaliwa na Halfani)