Loading...

Somalia yajiunga rasmi na umoja wa nchi za Afrika Mashariki

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: somalia-yajiunga-rasmi-umoja-nchi-afrika-mashariki-640-rickmedia

Nchi ya Somalia imekuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya kukamilisha hatua zote zilizohitajika ili kujiunga na Jumuiya hiyo

Sekretarieti ya EAC imechapisha taarifa inayoonesha Ujumbe wa Somalia ukikabidhiwa Hati yake ya Kuidhinishwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ikiwa ni utekelezaji wa Makubaliano yaliyoafikiwa Novemba 2023 na Wakuu wa Nchi nyingine za EAC.

Somalia inakuwa mwanachama wa nane wa EAC ikiungana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda.