Waziri Mkuu wa Israel Hoi baada ya kula chakula chenye Sumu

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 days ago
rickmedia: waziri-mkuu-israel-hoi-baada-kula-chakula-chenye-sumu-665-rickmedia

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alizidiwa kutokana na matatizo ya tumbo yaliyosababishwa na sumu ya chakula, ofisi yake ilisema Jumapili, ikiongeza kuwa ataendelea kutekeleza majukumu yake huku akipumzika nyumbani kwa siku tatu zijazo, kwa mujibu wa taarifa ya Reuters.

Netanyahu aliwahi kuwekewa kifaa cha kusawazisha mapigo ya moyo mwaka 2023, na Desemba mwaka jana alifanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume baada ya kugundulika kuwa na maambukizi katika mfumo wa mkojo yaani UTI.