Mike Tyson Afunguka Kwa Mara Ya Kwanza Tangu kupata Tatizo la Kiafya kwenye Ndege.

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 months ago
rickmedia: mike-tyson-afunguka-kwa-mara-kwanza-tangu-kupata-tatizo-kiafya-kwenye-ndege-69-rickmedia

#MikeTyson amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kupatwa na dharura ya kiafya na kupatiwa matibabu akiwa kwenye Ndege.

Kupitia ukurasa wake wa X, #Tyson amesema kuwa kwa sasa yupo vizuri asilimia 100 japo kuwa hataki kumpiga #JakePaul licha ya pambano hilo kutokufutwa kutokana na tatizo la kiafya la #Tyson.

"Sasa ninahisi nipo fiti asilimia100 ingawa sihitaji kumpiga Jake Paul," Tyson aliandika kwenye X wakati akirejelea pambano lake lijalo na Bondia #JakePaul.

Tyson alijihisi kupatwa na kichefuchefu na kizunguzungu wakati ndege ikitua akitokea Miami kwenda Los Angels hali iliyopelekea kupatiwa matibabu ya dharura ndani ya ndege.

Tyson, ambaye alimaliza maisha yake ya ndondi mwaka wa 2005, alikuwa ameratibiwa kurejea kwa ajili ya mechi iliyotarajiwa dhidi ya #Paul mwezi ujao.

Chapisho la hivi majuzi la #Tyson kwenye mitandao ya kijamii linathibitisha kwamba pambano hilo na #Paulhalitafutwa kutokana na tukio hilo la kiafya.