Mwanaume wa Kijapani ambaye alitumia $14k- Tsh.Milioni 36.4+ kujibadilisha kuwa mbwa anataka kutimiza ndoto nyingine ya kuwa mnyama tofauti.
Mwanamume huyo anayejulikana kama #TocoTheHumanCollie, alisema matatizo ya kusafiri kama mbwa yamemfanya afikirie kujibadilisha kuwa wanyama wengine.
Toco alifafanua zaidi kuwa mbwa na wanadamu wana muundo tofauti wa mifupa na harakati, kwa hivyo alikumbana na ugumu wakati wa kusafiri na harakati nyingine huku akidai kuwa anatamani kutimiza ndoto yake nyingine ya kujibadilisha na kuwa mnyama tofauti na Mbwa.
Hata hivyo, gazeti la New York Post liliripoti kuwa haijafahamika iwapo ana mipango ya mara moja ya kuiga wanyama wengine. Toco pia anaandika maisha yake ya kila siku akiwa amevalia mavazi kwenye YouTube na anakiri kwamba anakabiliwa na ukosoaji kwa mtindo wake wa maisha usio wa kawaida.