Imani ya Chris Brown kuhusu utajiri iko tofauti na watu wengine, yeye haamini kwenye utajiri wake binafsi bali anaamini kwenye utajiri wa vizazi vyake na hii inamfanya atofautiane na watu wengi kwenye imani hii
Kupitia Instastory yake Chris Brown ameandika “I don’t wanna be rich, I wanna create generational wealth.” kwamba hatakikuwa tajiri bali anataka kutengeneza kizazi cha utajiri.

Breezy mwenye upendo mkubwa kwa watoto wake 3, ameonekana wazi kuwa anawaza kuwajengea maisha mazuri ya huko mbele waendako kwani ameanza kwa kuwaweka karibu wote watatu (Ambao kila mmoja ana mama yake) anawafundisha upendo, lakini pia mara kadhaa huwachukua na kwenda nao kwenye show zake (Anawafundisha Uchapa kazi).
Kwa upande wa mashabiki wa Team Breezy, ujumbe huu ni kama mwendelezo wa safari yake kutoka kuwa dansa mwenye kipaji, hadi kuwa mmoja wa wasanii wanaoheshimiwa zaidi duniani, sasa akiyatafsri maisha nje ya muziki.