Staa wa Muziki #DiamondPlatnumz Amefunguka kuwa sababu kubwa inayomfanya kuwekeza kwenye mambo mbalimbali Nje ya Muziki ni kutokuamini Biashara ya Muziki.
Kwenye Mahojiano Na #Revolt, #Diamond Amezitaja Biashara zake njee ya Muziki huku akisema kuwa anawekeza kote huko kwa sababu Biashara ya Muziki haieleweki na itabaki kama kitovu chake cha Mafanikio.
Diamond Platnumz (jina halisi Naseeb Abdul Juma Issack) ni msanii wa Bongo Flava kutoka Tanzania. Yeye ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Wasafi Bet na Wasafi Media. Amekuwa maarufu Afrika Mashariki na Kati, na alikuwa msanii wa kwanza barani Afrika kufikisha watazamaji milioni 900 kwenye YouTube. Mwaka 2017 alisaini mkataba na Universal Music na kutoa albamu A Boy from Tandale mwaka 2018. Mwaka 2021, aliingia ubia na Warner Music Group kupitia lebo yake ya WCB Wasafi.