Staa wa Muziki #Nandy Amwaga Malalamiko kwa #MrTongeNyama ambae alidai kuwa Jina lake limetumika na Msanii #Nandy bila ridhaa yake hivyo anataka alipwe Kiasi cha Pesa cha Tsh.Milioni 200.
Kupitia ukurasa wa #Nandy Ameandika..
“BRO NAANDIKA KWA UCHUNGU SANA NALIA KWA HASIRA SANA. NILIKAA KIMYA ILI USHAURIANE NA LAWYER WAKO KAMA MKO SAHIHI SABABU MLINIPA BARUA NIKIWA NIMEWEKA VIDEO TU YA WATOTO WANAKULA MKASEMA NIMETUMIA JINA LAKE KWA FAIDA ZANGU BILA KUJUA NI WIMBO! WIMBO UMETOKA NIKAJUA MTAKAA CHINI MUELEWE KUWA SIKUWA NA NIA YA ILO MNALOSEMA JINA LENU BALI NIME FANYA SANAA KAMA WATU WENGINE KUMBE HAMKUTOSHEKA? KAKA MMENDA KUFUTA WIMBO WANGU YOUTUBE? INVESTMENT YANGU YOTE MNATAKA IZIMA SABABU UNAITWA TONGE NYAMA? MMENIKOSEA NILITEGEMEA WEWE NI KIJANA UNATAFUTA BASI KILA MTU ATAFUTE KWA AMANI ILA HUKUTAKA IVYO UMETAKA NIUMIE NIRUDI NYUMA! HII SIWEZI VUMILIA WE ARE DOING TOO MUCH WE ARE INVESTING TOO MUCH SIJUI KAMA HATA UNAELEWA DAAH! ACHA LAWYERS WETU WAONGEE ILA ASANTE.”