Kamala Harris Hatagambea Tena Ugavana

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: kamala-harris-hatagambea-tena-ugavana-457-rickmedia

Makamu wa Rais wa Zamani wa Marekani Kamala Harris Ametangaza kwamba hatagombea nafasi ya Ugavana wa California mwaka 2026, akiweka kikomo cha uvumi kuhusu nia yake ya kugombea nafasi hiyo lakini pia akifungua ukurasa mpya wa maswali kuhusu mipango yake ya baadaye baada uteuzi wa urais wa chama cha Democratic mwaka 2024.

“Kwa sasa, uongozi wangu na huduma yangu kwa umma haitakuwa katika nafasi ya kuchaguliwa,” alisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano.

“Kwa sasa, uongozi wangu na huduma yangu kwa umma haitakuwa katika nafasi ya kuchaguliwa,” alisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano. 

“Ninatarajia kurejea kwa wananchi, kusikiliza maoni yao, kusaidia kuwachagua wanademokrasia kote nchini watakaopigana bila woga, na kushiriki maelezo zaidi katika miezi ijayo kuhusu mipango yangu binafsi.”

Baada ya kushindwa kwake na Rais Donald Trump, Harris na timu yake walieleza kuwa atachukua muda kutafakari hatua zake zinazofuata, ambazo zilijumuisha kuzingatia kugombea Ugavana wa California au uwezekano wa kugombea tena urais mwaka 2028.