Watu 22 wamefariki na wengine 197 kujeruhiwa kufuatia maandamano nchini Angola

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: watu-wamefariki-wengine-197-kujeruhiwa-kufuatia-maandamano-nchini-angola-930-rickmedia

Watu 22 wamefariki na wengine 197 kujeruhiwa kufuatia maandamano nchini Angola kupinga kupanda kwa bei ya mafuta. 

Serikali ilipandisha bei ya mafuta yenye ruzuku kutoka Kwanza 300 hadi 400 (takribani euro 0.28 hadi 0.38) kwa lita, hali iliyozua hasira kwa wananchi.

Licha ya kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika baada ya Nigeria, idadi kubwa ya Wanaangola wanaishi katika hali ya umasikini.

Awali, mashirika ya kiraia yalitisha maandamano ya kila Jumamosi, lakini hali ilizidi kuwa tete baada ya chama cha madereva wa teksi kutangaza mgomo wa siku tatu kuanzia Jumatatu Hali iliyosababisha kutokea kwa uporaji kwenye maduka ya miji kadhaa.

Serikali haijatoa tamko rasmi kuhusu kupunguza bei hizo huku hali ya usalama ikiendelea kuwa tete.