Dulla Makabila ashindwa kujizuia kufanya shows kipindi cha Ramadhan

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: dulla-makabila-ashindwa-kujizuia-kufanya-shows-kipindi-cha-ramadhan-253-rickmedia

Kuna msemo huwa unasema "Majaribu hayana budi kuja" msemo huu huenda ukawa unamuhusu Dulla Makabila moja kwa moja kutokana na majaribu anayoyapitia kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan Dulla anasema mpaka sasa ametafutwa kwaajili ya show 6 na nyingine zinazidi kumiminika na kila akikataa kwamba afanyi show mwezi huu wanamuongezea malipo.

Dulla amemaliza kwa kuamua kuwa atafanya show hizo ila Mungu amsamehe kwasababu hata kipaji hicho ni yeye aliyempatia, naamini sio Dulla tu ambaye anapata show hizo kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan,ni wasanii wengi na wengi wao wanazikataa kutokana na utaratibu waliojiwekea katika mwezi huu japo huwa hawazungumzii mitandaoni.