Jared Leto Ashtakiwa na Wanawake 9 kwa Tabia za Kingono

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

3 days ago
rickmedia: jared-leto-ashtakiwa-wanawake-kwa-tabia-kingono-923-rickmedia

Mshindi wa Tuzo ya Oscar #JaredLeto ameshtakiwa na wanawake tisa kwa mienendo isiyofaa, huku baadhi yao wakielezea tabia ya mwanamuziki huyo na muigizaji mwenye umri wa miaka 53 ya kuwafanyia vitendo vya Kingono kipindi wanamiaka 16.

Katika ripoti mpya iliyochapishwa na #AirMail siku ya Jumamosi, Juni 7, wanawake tisa wamejitokeza wakimtuhumu #Leto kwa tabia zisizofaa katika kipindi cha miaka mingi, ikiwa ni pamoja na kufanya vitendo vya kingono vijana wa kike.

Mwakilishi wa #Leto alikana vikali tuhuma mbalimbali zilizoripotiwa na Air Mail, ikiwa ni pamoja na zile za Teilz, ambazo walisema ni za uongo wa wazi.

Muda mfupi baada ya habari hizo kusambaa, Jared Leto alikanusha madai ya tabia mbaya ya kingono ya muda mrefu yaliyoibuliwa na wanawake hao, akiwemo DJ na mtayarishaji wa muziki Allie Teilz, aliyefufua madai yake ya zaidi ya miaka kumi dhidi ya muigizaji huyo.

Mwakilishi wa Leto aliambia Air Mail, Madai yote yanakanushwa waziwazi.