Rapa Wa Marekani Jcole Tayari Ameiondoa Diss Track Yake “7 Minute Drill” Katika Platform Zote Za Kusikiliza Muziki Baada Ya Kumuomba Msamaha Kendrick Lamar Katika Tamasha La Dreamville Wiki Iliyopita.
Wiki Iliyopita Jcole Katika Tamasha La Dreamville Aliomba Radhi Kwa Kendrick Na Kudai Kuwa Amejutia Kum-Diss Katika Ngoma Yake Ya “7 Minute Drill” Na Hivyo Alitamani Kuiondoa Kabisa Kwenye Streaming Platforms Zote, Ambapo Kwasasa Tayari Amefanya Hivyo.
Katika Diss Track Walizojibizana Wawili Hao Walitambiana Huku Kila Mmoja Akidai Ni Mkubwa/ Mkali Kuliko Mwenzake. Ambapo Mwaka Huu Kendrick Alianza Kwa Kujibu Diss Ya Drake & J. Cole ‘First Person Shooter’ ambapo kwa pamoja walimchana Kendrick kuwa hayupo kwenye orodha ya rappers wakali, na kwenye ile Big 3 (Drake, J. Cole & Kendrick) kwa sasa wamebaki wawili tu Yani J Cole Na Drizzy.
Ndipo Kupitia Ngoma Ya Future “Like That” Kendrick Aliibuka Na Kujibu Kuwa yeye ni mkali kuliko wao (J cole & Drizzy) “/Motherf*ck the Big 3, n***a, it’s just big me.”
Badae J.COLE Nae Akajibu Kwenye “7 Minute Drill” Kwa Kusema Mwamba bado anafanya shows lakini zinabuma Yani Mikosi, Album yake ya kwanza (Section.80) ilikuwa kali lakini ya mwisho (Mr. Morale & the Big Steppers) ni msiba! bora hata (To Pimp a Butterfly) ambapo J. Cole alisema huo ndio ulikuwa wakati wa Kendrick Lamar!.