Jinsi Justin Bieber Alivyotumia Vibaya Zaidi Trilioni 2 Mpaka kuelekea Kufilisika

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 weeks ago
rickmedia: jinsi-justin-bieber-alivyotumia-vibaya-zaidi-trilioni-mpaka-kuelekea-kufilisika-653-rickmedia

Staa wa muziki #JustinBieber alitengeneza kati ya dola milioni 500 hadi bilioni 1 akiwa nyota mkubwa zaidi wa muziki duniani, lakini alitumia pesa hizo zote vibaya na akaishia kuwa katika hali mbaya sana ya kifedha kiasi kwamba alilazimika kuuza katalogi yake ya muziki kwa dola milioni 200.

#TMZ ina makala mpya ya uchunguzi inayoitwa "TMZ Investigates: What Happened to Justin Bieber," sasa inapatikana kwenye Hulu, na sehemu ya uchunguzi wao inachunguza matatizo ya kifedha ya #Justin.

Watu walioko upande wa #Justin wamefunguka kwamba alikuwa karibu kufilisika kabisa mnamo mwaka wa 2022 kiasi kwamba alihisi kulazimika kuuza haki za muziki wake mwezi Desemba mwaka huo.

Meneja wa #Justin, #ScooterBraun, alijaribu kumshauri kuwa ni wazo mbaya kuuza mapema katika taaluma yake, na kwamba angalau asubiri hadi Januari 2023 ili apate nafuu ya kodi lakini #Justin hakutaka kusubiri, hivyo akauza mwezi Desemba.

Wasanii wengi wameuza katalogi zao, lakini Justin ndiye msanii mwenye umri mdogo zaidi kufanya hivyo na waliweka wazi kuwa hali mbaya kifedha ilichangia sana uamuzi wake.

Makala hiyo kuhusu Bieber pia inachunguza afya yake ya akili, ndoa yake, matatizo yake ya kifedha, kanisa lake na taaluma yake ya muziki.