Lebo ya Universal Music iliacha kufanya kazi na Liam Payne kabla ya kifo chake

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 days ago
rickmedia: lebo-universal-music-iliacha-kufanya-kazi-liam-payne-kabla-kifo-chake-836-rickmedia

Msanii wa zamani wa One Direction, Liam Payne, ameripotiwa kufariki kwa kuanguka kutoka gorofa la tatu katika hoteli ya CasaSur Palermo, Buenos Aires, Argentina. Tukio hilo lilitokea Jumatano jioni huku Payne akiwa amekuwa na tabia ya kuharibu vyumba vya hoteli na kufanya vitendo vya utata kabla ya kifo chake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Universal Music walimfuta Liam Payne kwenye orodha yao ya wasanii siku chache kabla ya tukio hilo kutokana na changamoto za muziki wake, ambao ulikuwa hauendelei vizuri. Uvumi wa changamoto za kisheria na matatizo ya mahusiano yake na mpenzi wake wa zamani, Maya Henry, ziliongeza shinikizo kwa msanii huyo kuwa na tabia za ajabu, Liam pia alisemekana kuwa na changamoto za afya ya akili.

Universal Music ilitoa salamu za rambirambi, ikisema kuwa "urithi wake utaendelea kuishi kupitia muziki wake na mashabiki wengi aliowatumikia."