WHO: Takribani watu 30,000 wamepata Mpox Afrika

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 weeks ago
rickmedia: who-takribani-watu-30000-wamepata-mpox-afrika-781-rickmedia

Ripoti ya Shirika la Afya kuhusu hali ya maambukizi ya Ugonjwa wa MPOX Barani Afrika, imeeleza kuwa zaidi ya Watu 812 wamefariki kwa Ugonjwa huo.

Pia, Wagonjwa wapya 2,082 wameripotiwa katika kipindi cha Mwezi Agosti, 2024 pekee huku Nchi za DR-Congo na Burundi zikiendelea kupata visa vipya

Aidha, Mfuko wa Benki ya Dunia wa Kusaidia Majanga umesema utatoa Dola za Marekani Milioni 128.89 (Takriban Tsh. Bilioni 351.86) kwa nchi 10 za Afrika ili kukubiliana na maambukizi ya Ugonjwa huo.