Mahakama yasitisha kwa muda kuondolewa kwa Gachagua Mahakamani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: mahakama-yasitisha-kwa-muda-kuondolewa-kwa-gachagua-mahakamani-464-rickmedia

Mahakama Kuu imesitisha uamuzi wa Seneti wa kuidhinisha hoja ya kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua lililofanyika Oktoba 17, 2024.

Uamuzi huo umetolewa Oktoba 18, 2024 na Jaji Chacha Mwita baada ya Mawakili wa Gachagua kuwasilisha ombi la kuzuia Rais William Ruto kuteua Mtu atakayejaza nafasi ya Naibu Rais baada ya Gachagua kuvuliwa Madaraka na Bunge la Seneti.

Aidha, Wabunge wa Kenya wamepiga kura ya kuridhia Prof. Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais kwa kura 236 huku kukiwa hakuna kura ya Hapana wala iliyoharibika