Mahakama kuu ya Mpumalanga nchini Afrika Kusini Jumanne ilimhukumuMzee mwenye umri wa miaka 51, #JosayaNdlozi, kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya mpenzi wake, #SophiePhumzileMalele, baada ya kumshtumu kwa kumsaliti.
Mshtakiwa alitangazwa moja kwa moja kuwa hafai kumiliki silaha kwa mujibu wa Kifungu cha 103 cha Sheria ya Kudhibiti Silaha namba 60 ya mwaka 2000.
Mahakama ilisikia kwamba mshtakiwa na marehemu walikuwa wakiishi pamoja huko Lydenburg na walikuwa na watoto watatu pamoja.
Kabla ya tukio hilo, #Malele aliomba hati ya ulinzi ya muda dhidi ya #Ndlozi na mojawapo ya masharti hayo ni mshitakiwa kutomvamia, kumtishia, wala kumnyanyasa marehemu kwa kuwa uhusiano wao ulikuwa tete.
Asubuhi ya tarehe 08 Februari 2023, watoto hao walikuwa shuleni na mabishano kati ya mshtakiwa na marehemu yakazuka.
Iliongezeka na kupelekea mshitakiwa kumchoma kisu Malele sehemu ya juu ya mwili wake na kuanguka.
Baada ya kugundua kuwa Malele hasogei, alitoa taarifa kwa jirani yake mmoja na polisi.
Malele alitangazwa kufariki eneo la tukio na mshitakiwa alikamatwa. Sababu ya kifo cha Malele ilikuwa majeraha mengi makali kwenye shingo.