CP Haji: Baadhi ya vyama kudai vinakandamizwa na Jeshi la Polisi ni dhana potofu

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 days ago
rickmedia: haji-baadhi-vyama-kudai-vinakandamizwa-jeshi-polisi-dhana-potofu-146-rickmedia

Kamishina wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Awadhi Haji amesema Jamii inatakiwa kuachana na dhana kuwa Jeshi hilo linakandamiza baadhi ya Vyama vya Siasa badala yake itambulike wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria

Amesema "Mfano kuna Watu wanafanya maandamano yaliyokataliwa kwa mujibu wa Sheria, Jeshi la Polisi lazima lichukue hatua, hivyo katika utekelezaji huo wanaona wanakandamizwa, itambulike kuwa Haki lazima iendane na Wajibu.

Ameyasema hayo wakati akishiriki mafunzo ya kukumbushana Sheria na miongozo mbalimbali kwa Makamanda wa Jeshi la Polisi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, ambapo mafunzo hayo yanaratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).