META yawafuta kazi walionunua mahitaji yao mengine kwa pesa ya chakula

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: meta-yawafuta-kazi-walionunua-mahitaji-yao-mengine-kwa-pesa-chakula-891-rickmedia

Kampuni ya META imewafukuza Wafanyakazi zaidi ya 24 ambao walibainika kutumia Fedha ziliwekwa kwenye Kuponi za Chakula wakiwa kazini na kununua Mahitaji mengine zikiwemo Sabuni za Kufulia na Dawa za Meno.

META imesema imechukua uamuzi huo kwa Wafanyakazi wa WhatsApp, Instagram na Facebook ambao wamekuwa wakitumia kinyume na makubaliano marupurupu, pia imewahamisha vitengo wengine.

Kampuni hiyo imekuwa ikitoa Chakula bure kwa Wafanyakazi katika Migahawa ya Ofisi za Silicon Valley, na walio nje ya ofisi hupewa Dola 70 (takriban Tsh. 190,750) kila siku kwaajili ya Huduma hiyo kila siku.